Kwanza kabisa kanzu Zetu zinashona Oman kwa Mafundi waliobobea kwenye kazi hii na Yenye Ubora na umaliziaji wa Ufumwaji vizuri. Pili kanzu tunaleta za Tayari ambazo zimeshona kwa Vipimo Tofauti Vipimo vya mtoto umri wa Mwaka mmoja mpaka mtu mzima. Tunaleta za vipimo vya watu wembamba (slim fit) , watu wa kati ( medium size) na pia watu wanene ( big size) Tatu pia huwa tunapokea Oda maalum ( special orders) kwa wale wenye uhitaji binafsi na matakwa Binafsi na kwa Machaguo maalum watakavyo ( customized orders)
unatoa huduma za Kuwavalisha Maharusi kwa utamaduni wa Ki Omani, emarati na hata Kwa utamaduni wa Kizanzibari pia. ila sana tumebobea kwenye Uvalishaji Asili ya Oman. Utaratibu ni wa Kuja Kuchagua Vilemba,na jambia au kupanga na bakora utazohitaji kwa siku yako ya harusi, utapata kuchagua rangi ya kilemba na Joho utakalo na kuweka Miadi (booking) ya tarehe. kwa huduma hizo Pekee Na Ubora wa hali ya juu hakuna pengine pa kuzipata zaidi ya ALHINAI CLASSIC kwani mteja wetu ni zaidi ya MFALME.

